Thursday, April 16, 2015

YERICKO NYERERE: AGALIZO KWA WANAONUIA UONGOZI WA KISIASA


UONGOZI WA KISIASA

Siasa ni itikadi inayofuatwa na kundi au jamii fulani ambayo ni msingi wa kuendesha uchumi, utamaduni na mwenendo mzima wa maisha ya jamii hiyo. Siasa sio ile ya "mchezo mchafu" kama umma ulivyo aminishwa.

Mwezi wa kumi mwaka huu tunaingia kwenye uchaguzi mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais,

Kwa sasa Tanzania ina wanasiasa wachache sana hawazidi wanne ama kumi, wengi wao ni wajasiliasiasa. Kwao siasa ni uwaniaji wa madaraka nakisha kuingia madarakani kuchuma/kuiba mali za umma tu.

Nitoe rai kuwa sasa ufike wakati wakutumia siasa za kisasa, siasa zinazokaa kwenye maandishi na sio za kuamini maalbino ndugu zetu.

Kwa mda uliosalia unatosha kuwa na mipango/mpango thabiti wa ushindi kisiasa ulioandaliwa na wataalumu kitaalamu, tunao wasomi wazuri waliobobea kwa kazi ya mipango mikakati ya kisiasa, hebu watumieni muone matunda yao, wamesoma kwaajili hiyo, nawengine serikali imewasomesha kwaajili hiyo lakini hawatumiki, wanasiasa mnakwenda kwa mazoea wakati wataalamu wapo??

Kuna faida nyingi kutumia wataalamu wa siasa,

1. Unapata kujitathimini nguvu yako kisiasa, kutambua aina ya ushindi utakaopata,

2. Kupunguza gharama za kampeni kwakupunguza masuala yasiyo na msingi, kujua gharama halisi za kampeni zako mpaka siku unaapishwa,

3. Kupunguza vifo vya maalbino (kama wapo watumiao).

4. Kujengwa kitaalamu namna ya kutoa hotuba thabiti za kampeni, kuwa na sera na agenda za kitaalam zihusuzo mahitaji ya umma wa eneo unalowania kugombea.

5. Kukabiliana na wapinzani wako ndani ya chama bila kuathiri taasisi (chama), kujua nguvu ya mpinzani wako rasmi (wa chama kingine) na udhaifu wake.

6. Kuiandaa mioyo yenu (nafsi) kushinda ama kushindwa. Hili linapunguza msongo wa mawazo na kifo baada ya uchaguzi hasa kama utashindwa.

Achaneni kuishi kwa mazoea, tumieni wataalamu waliopo kila pembe ya nchi

No comments: