Tuesday, April 14, 2015

UMUHIMU NA NAMNA YA KOTO FAUT I SH A BIASHARA KWENYE MAISHA

Kwa wafanya biashara wa aina yoyote

Mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA
tumekutana tena leo kwenye kipengele hiki cha
USHAURI WA CHANGAMOTO mbalimbali ambazo
zinatuzuia kufikia malengo yetu na hatimaye
mafanikio makubwa kwenye maisha. Maisha yana
changamoto nyingi sana na wakati mwingine
unaweza usione kipi sahihi cha kufanya hasa
unapokuwa katikati ya changamoto hizi. Ni
kupitia kipengele hiki ambapo tunaweza
kusaidiana mawazo na hatimaye ukaweza
kutatua changamoto yako.
Leo tutaangalia changamoto ya kutofautisha
biashara na maisha ya kawaida. Hii ni
changamoto kubwa sana na ambayo imewafanya
wengi washindwe kufikia mafanikio kupitia
biashara zao.
Mara nyingi watu wanapopata matatizo kwenye
maisha, huona biashara zao ni sehemu rahisi
kwao kutatua matatizo yao. Tatizo kubwa
linakuja kwamba mtu anapotumia biashara yake
kutatua matatizo ya maisha, matatizo hayaishi
na biashara inaathirika sana na hata kufa kabisa.
Hata watu wanaosema kwamba kuna chuma
ulete kwenye biashara zao, wao wenyewe ndio
chuma ulete kwa sababu wanashindwa
kutenganisha biashara na maisha yao ya
kawaida. Unapochanganya biashara na maisha
ya kawaida huwezi kuona maendeleo makubwa
kwenye biashara yako.
Je ufanye nini ili uweze kutofautisha maisha ya
kawaida na biashara ili uweze kuona mafanikio
kwenye biashara yako?
Kabla hatujaona nini cha kufanya, tuone maoni
ya msomaji mwenzetu kuhusu swala hili.
Changamoto yangu ni kwamba: najihusisha na
biashara ya nafaka(mahindi na mpunga).
Nikiweka stoo kwa ajili ya kuuza baadae ili
nipate faida,hali ya hewa inakuwa mbaya kama
vile ukame na njaa hali inayopelekea kuwagawia
tena ndugu zangu kiasi fulani cha hiyo stoo
maana wananitegemea sana. Nikiuza kilichobaki
hakinipi faida zaidi ya gharama za kununulia tu.
Je nifanyeje?
Tumeona maoni ya msomaji mwenzetu juu ya
muingiliano wa biashara yake na maisha ya
kawaida. Inawezekana hata wewe kuna jinsi
ambavyo biashara yako inaingiliana na maisha,
kwa mfano matumizi yako yanatoka moja kw
amoja kwenye biashara na vingine vingi.
Vifuatavyo ni baadhi ya vitu unavyoweza kufanya
ili kutatua changamoto hii.
Kwanza kabisa ni muhimu utambue
kwamba tatizo la njaa linalotokea
halitokei kwa sababu wewe una akiba y
chakula. Na hata linapotokea na kama
usingekuwa na akiba ya chakula, bado
watu wangepata njia ya kutatua tatizo
hilo. Ila kwa sasa hawafikirii sana njia
nyingine kwa sababu wana uhakika
kwamba wewe utakuwa na chakula
wakati huo wa njaa na utawasaidia. Hii
hali ya kawaida kwa binadamu, hatupen
kujichosha sana ahasa tunapokuwa na
uhakika na kitu. Kikubwa cha kufanya
hapa ni wewe kuwahamasisha hao ndug
zako watunze mazao ya kutosha wakati
wa msimu wa mavuno, na uwaambie
wazi kabisa kwamba mazao unayonunu
wewe na kutunza sio kwa ajili ya
chakula, bali ni kwa ajili ya biashara.
Kwa hali hii utawafanya waanze
kuchukua majukumu ya maisha yao na
kuacha kuwa tegemezi. Najua unaweza
kufikiria kwamba kufanya hivyo
utaonekana una roho mbaya, ila ukweli
kwamba unahitaji kuchagua kitu kimoja,
kuonekana una roho nzuri, huku biashar
yako inakufa na unaendelea kulalamika
moyoni au kuonekana una roho mbaya,
huku ukiwasaidia watu kuchukua
majukumu ya maisha yao na wewe
biashara yako kukua. Hii pia unaweza
kuitumia kwenye biashara ya kawaida,
unapopata matatizo, mawazo yako ya
kwanza yasiwe kwenye biashara yako,
fikiria njia nyingine kwanza za kutatua
tatizo hilo. Lazima kuna njia nyingi tu,
hasa pale unapofikiria kama nisingekuw
na biashara hii ningefanya nini?
Pili , badili mipango na muundo wako w
biashara. Kama unaona kufanya hiko
nilichoshauri hapo juu ni kigumu kwako,
basi unaweza kubadili muundo na
mipango ya biashara yako. Kwa mfano
badala ya kusubiri mpaka kipindi
ambacho hakuna kabisa mazao ndio
uuze, uza mapema kabla njaa haijaanza.
Hata kama hutouza kwa bei kubwa san
fanya hivyo ili kuepuka kukosa kabisa
faida. Kumbuka hufanyi hivi ili
kuwanyima ndugu zako chakula, ila
unafanya hivi ili kuokoa biashara yako,
ambayo kama ikikua, utaweza
kuwasaidia hao ndugu zako zaidi.
Angalia jinsi utakavyoweza kuuza maza
yako mapema kabla ya njaa kuingia na
kulazimika kuwagawia ndugu zako na
wewe kushindwa kupata faida.
Tatu , nunua mazao ya ziada wakati wa
mavuno. Kitu kingine muhimu
unachoweza kufanya, ni kununua maza
ya ziada wakati wa msimu wa mavuno.
Fanya hivi ukilenga kuweka sehemu ya
mazao hayo kama chakula pale njaa
itakapotokea. Na njaa itakapotokea
hakikisha unagawa kiasi kile cha ziada
ulichonunua tu, kikiisha unawaambia
ukweli kwmaba kimekwisha na waangali
njia nyingine za kuokoa maisha yao.
Nne badilisha biashara kabisa. Kama
hayo yote tuliyojadili hapo juu
hayatawezekana kwenye hali yako,
unachiweza kufanya ni kubadili biashara
kabisa. Angalia ni biashara gani
utakayoweza kufanya kwa maeneo
uliyopo ambayo haitakuw ana muingilia
mkubwa sana na watu kiasi cha wao
kukutegemea sana wewe. Ukifikiria vizu
hutakosa biashara ya tofauti. Kuliko
kufanya biashara moja ambayo
haikupeleki mbele miaka yote ni bora
kubadili na kuangalia biashara nyingine
ambayo inaweza kukupa nafasi nzuri ya
kuendelea.
Kikubwa nachoweza kukushauri kwa ujumla ni
kwamba unahitaji kuwa makini sana na biashara
yako. Watu wakishajua sehemu fulani
kunapatikana suluhisho la matatizo yao,
hawafikirii tena kitu kingine. Ni bora uamue
kufanya maamuzi magumu ya kukuza biashara
yako kwa njia tulizojadili hapo juu hata kama hao
ndugu zako watakuona mbaya, ila biashara yako
itakapokuwa utaweza kuwasaidia vizuri zaidi
ikiwepo hata kuwapatia kazi mbalimbali. Lakini
ukiendekeza hili la njaa, mtazidi kurudishana
nyuma na hutawez akuwasaidia vizuri.
Kumbuka njia nzuri ya kumsaidia masikini ni
wewe kutokuwa masikini, ukikubali kuendelea
kuunganisha biashara yako na maisha,
utaendelea kuwa masikini na hutaweza
kuwasaidia hao ndugu zako.
Nakutakia kila la kheri kwenye kutenganisha
biashara yako na maisha ya kawaida.

No comments: